Azalea Banks anasema kipengele cha tuzo za BET kwa Female Rap ni utani, Inafurahisha sababu anaweza akawa sawa, lakini pointi yake ya msingi ni kwamba Nicki Minaj anawekwa kila mwaka na anashinda.
Anasema anachukia kuchaguliwa kushiriki tuzo za BET kwa sababu ni mafala sana, na wanaendelea kukosea kuandika jina lake.
Aliendelea kuchana kwa kusema watamuweka Nicki Minaj mara tano na picha tano tofauti akiwa amebadilisha wig mara tano.
Unadhani msanii yeyote wa kike anaweza kushindana na Nicki Minaj?
Nini kilitokea kwa wasanii wa kike waliopo sasa kwenye Hip Hop? Nini kilitokea kwa wasanii wakali wa kike?
Angalia Tweets za Azalea Banks.
Ni maoni yake tu, freedom of speech, xpress yourself, kwa sababu hata Tanzania tumeshuhudia watu kulalamika kwa ishu kama hizi.
Lakini yeye anaona kila mwaka anawekwa Nicki Minaj na anashinda anaona kama wanachemka jamaa.
Unasemaje as a music fan?